Thursday, September 21, 2023
No menu items!
HomeSportsWachezaji wa Simba SC kabla ya mechi yao dhidi ya Azam FC...

Wachezaji wa Simba SC kabla ya mechi yao dhidi ya Azam FC jana

SIMBA wamekiri msimu huu hata nafasi ya pili wanaweza wasiipate lakini wakasema: “Tutakufa na Yanga.”
Mabingwa hao watetezi wamekuwa na mwendo wa kusuasua tangu kuanza kwa msimu huu. Kabla ya mechi ya jana, walikuwa katika nafasi ya nne, nyuma ya Kagera Sugar, Azam na Yanga.
Kocha msaidizi wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, amesema kwa sasa wanacheza ili kulinda heshima ya Simba tu. SIMBAGPL
Amesema ni lazima washinde mechi dhidi ya Yanga (ya mwisho) itakayochezwa Mei 18, mwaka huu, kwa kuwa ndiyo itakayowapa heshima kwa wanachama wao.
“Simba sasa tunatengeneza timu mpya kwa ajili ya ligi ya mwakani, hatupo tena katika mbio za ubingwa, lakini sasa tunachofanya ni kulinda heshima ya timu katika michezo iliyosalia, tumejipanga kuhakikisha tunashinda michezo yote.
“Lakini kikubwa zaidi ni mchezo dhidi ya Yanga, tumewaambia wachezaji dhamira yetu juu ya mchezo huo kwamba ushindi ni lazima, lakini pia na wao wanatakiwa kujituma zaidi ili kuweza kujitafutia soko katika kipindi kijacho cha usajili,” alisema Julio.
Simba imeshatoka kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara, kwani hata kama ikishinda mechi zake zote nne zilizosalia, haiwezi kufikia pointi 52 walizonazo Yanga.

RELATED ARTICLES
- Advertisment -

Most Popular

Recent Comments