Na Khatimu Naheka
UONGOZI wa Toto African ya Mwanza, umekiri wazi kwamba timu yao ipo katika wakati mgumu katika kusalia Ligi Kuu Bara, lakini ukasema Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ndiyo tatizo.
Kauli hiyo ya Toto inakuja ikiwa imepita siku moja tangu ikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Kagera Sugar, huku timu hiyo ikikabiliwa na tatizo kubwa la ukata.
Mwenyekiti wa Toto, Omari Nosli, ameliambia Championi Ijumaa kuwa, TFF kupitia kamati yake ya ligi ndiyo kiini kikubwa kitakachoishusha timu yao, kutokana na upangaji mbovu wa ratiba ya ligi ambapo italazimu baadhi ya klabu kupanga matokeo.
Nosli alisema uongozi wa timu hiyo umeshangazwa na taarifa zilizokuwa zinatolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, Wallace Karia, ambapo amekuwa akidai uongozi wa Toto uliandika barua kuomba kuharakishwa baadhi ya michezo yake taarifa ambazo siyo za kweli.
“Ukiangalia msimamo wa ligi sasa, utaona kuna timu zimebakiza mechi tatu nyingine mbili, lakini ajabu kwetu tumebakiza mchezo mmoja pekee,” alisema Nosli.
Recent Comments